Posts

MACHAPISHO

ELIMU JUMUISHI NI NINI?

Image
ELIMU JUMUISHI         ni istilahi ambayo kwa miaka mingi nchini Tanzania ilitumika sana kumaanisha kuchanganya wavulana na wasichana katika muktadha wa ujifunzaji na ufundishaji na hasa wale wenye wenye ulemavu mbalimbali kama vile wasioona, viziwi n wenye ulemavu wa akili na viungo. Hata hivyo humaanisha kuwahusisha wasichan na wavulana wote ambao huachwa bila kuandikishwa au kutengwa na shule kwa sababu ya rangi, tamaduni, uchumi na hata maumbile.Hivyo basi, jumuishi ni namna ya kuongeza ushiriki katika tendo la ujifunzaji na ufundishaji miongoni mwa wanafunzi. Ushiriki huu situ kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum bali ni juu ya kubadili mtazamo hasi ambao unawatenga watu wenye ulemavu na mahitaji ya ujifunzaji na pia kukuza fursa sawa kwa wanafunzi wote. Jumuishi katika muktadha wa mwalimu ni kwamba tunawajibika kubadilisha mitazamo ya njia, mbinu na mikakati ya tendo la ujifunzaji na ufundishaji katka darasa jumuishi. Pia ni jukumu la mwalimu kutafuta msaada kat...