ELIMU JUMUISHI NI NINI?


ELIMU JUMUISHI

        ni istilahi ambayo kwa miaka mingi nchini Tanzania ilitumika sana kumaanisha kuchanganya wavulana na wasichana katika muktadha wa ujifunzaji na ufundishaji na hasa wale wenye wenye ulemavu mbalimbali kama vile wasioona, viziwi n wenye ulemavu wa akili na viungo. Hata hivyo humaanisha kuwahusisha wasichan na wavulana wote ambao huachwa bila kuandikishwa au kutengwa na shule kwa sababu ya rangi, tamaduni, uchumi na hata maumbile.Hivyo basi, jumuishi ni namna ya kuongeza ushiriki katika tendo la ujifunzaji na ufundishaji miongoni mwa wanafunzi. Ushiriki huu situ kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum bali ni juu ya kubadili mtazamo hasi ambao unawatenga watu wenye ulemavu na mahitaji ya ujifunzaji na pia kukuza fursa sawa kwa wanafunzi wote.


Jumuishi katika muktadha wa mwalimu ni kwamba tunawajibika kubadilisha mitazamo ya njia, mbinu na mikakati ya tendo la ujifunzaji na ufundishaji katka darasa jumuishi. Pia ni jukumu la mwalimu kutafuta msaada katika maeneo ya mamlaka za shule, jamii, taasisi za elimu watoto, huduma za afya na uongozi wa jamii ambao unazunguka shule ili kusaidia kuwapata wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na wasio na mahitaji hayo kwa urahisi. Hii itasaidia wototo wote katika jamii wenye umri wa kwenda shule kuandikiswa na kusoma kwa pamoja, hivyo ni wajibu wa mwalimu kufanya uchechemuzi chanya.


Dhana ya Elimu Jumuishi

Ni mfumo wa utoaji elimu ambao unatoa fursa ya elimu kwa watoto, vijana na watu wote bila kujali tofauti zao. Aidha ni mchakato wa kuongeza ushirikishwaji wa watoto wote shuleni ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu. Mchakato huu ni endelevu ili kubadili mila, desturi, fikra, imani, mtazamo, sera, mbinu na mazingira shuleni ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wanafunzi katika jamii. Vilevile huhusisha ubainishaji wa vikwazo vya ushirikishwaji katika tendo la ujifunzaji kwa wanafunzi wote. Mpango Mkakati wa Elimu Jumuishi (2009- 2017) pamoja na Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) zinabainisha umuhimu wa utekelezaji wa Elimu Ju


Sifa za Elimu Jumuishi

Mambo ya kuzingatia katika utoaji wa elimu jumuishi

Kuukubali uanuai.


Kuwa na mtizamo chanya kwa wenye mahitaji Maalum ikiwa ni pamoja kutowanyanyapaa kwa kuwaita majina ya kejeli.


Kuboresha na kufanya mazingira ya shule yawe rafiki kwa watoto wote.


Kuwawezesha walimu ili waweze kufanya kazi kwenye mfumo wa elimu jumuishi kwa kuboresha mbinu za ufundishaji.


Kuwa na Mazingira Jumuishi na Rafiki Katika UjifunzajiMaana ya mazingira jumuishiMazingira jumuishi na Rafiki ni yale yanayomfanya mtoto yeyote mwenye mahitaji na Maalum na asiye na mahitaji Maalum kuipenda shule na kufurahia tendo la ujifunzaji.Mtoto anapenda aende shule salama ,aishi na kujifunza kwenye mazingira yanayomfurahisha na kupata mahitaji yake yote ya kimwili na kiakili. Mambo ya kuzingatia katika kuandaa mazingira jumuishi na rafiki ya ujifunzajiNjia na mbinu nyumbufu za kufundishia na kujifunziaMitazamo mbalimbali ya wana jamiiMahusiano kati ya:- Walimu na  wanafunzi- Walimu na wazazi- Wanafunzi na wanafunzi- Wazazi na jamiiVifaa vya kufundishia na kujifunzia na visaidiziLugha ya kufundishiaTathmini na upimaji.Hatua za kuwa na mazingira jumuishi na rafiki ya ujifunzaji- kujenga mtazamo chanya kuhusu watoto wenye mahitaji Maalum kwa kutoa Elimu kwenye ngazi ya familia , jamii , watoto , walimu na wadau wote wa elimu.- kuboresha mazingira ya shule ili yawe jumuishi na rafiki yanayokidhi mahitaji ya wanafunzi wote.- Kuboresha sera na kanuni kuhusu Elimu jumuishi zinazolinda maslahi ya watoto wenye mahitaji Maalum zinaweza kuwa za kitaifa, kiwilaya, kikata na kishule.- kubadili mfumo wa uendeshaji wa shule kwa kurekebisha taratibu ili kutoa fursa zaidi katika utekelezaji wa Elimu jumuishi. Mabadiliko haya yanaweza kuhusisha mitaala, mafunzo ya ualimu vyuoni na kazini itakayowawezesha kutoa elimu kwa watoto wote.


Changamoto za uanzishaji wa elimu jumuishi

Mtazamo hasi wa baadhi ya wadau Watoto wengi wenye ulemavu kutokutambulika katika jamiiWatoto wenye mahitaji Maalum kutotambulika shuleniGharama za utoaji wa elimu Ukubwa wa madarasaUmasikiniUbaguzi wa kijinsiaUtegemezi wa watoto wenye ulemavuJinsi ya kukabiliana na uanzishaji/uendeshaji wa elimu jumuishiKujenga mtazamo chanya kuhusu watu wenye ulemavuKujenga mazingira jumuishi ya kujifunziaKuboresha sera/kanuni kuhusu elimu jumuishiKubadili mfumo wa uendeshaji wa shule.


Comments